Uhariri wa Wikipedia 101

Uhariri wa Wikipedia 101

Categories: Wikipedia
Wishlist Share
Share Course
Page Link
Share On Social Media

About Course

Maelezo ya Kozi:
Kozi ya Uhariri wa Wikipedia 101 inalenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa msingi wa kuhariri Wikipedia, jukwaa kubwa la maarifa ya wazi ulimwenguni. Katika kozi hii, wanafunzi watajifunza:

  • Namna ya kufungua na kusimamia akaunti ya Wikipedia.
  • Kanuni za msingi za kuhariri makala, ikijumuisha kuongeza, kuhariri, na kufuta taarifa n.k.
  • Matumizi ya viwango vya uandishi na marejeleo sahihi ili kuhakikisha ubora wa maudhui.
  • Mbinu za kushirikiana na wanajamii wengine wa Wikipedia kwa njia ya kujenga.
  • Utambuzi wa sera na miongozo muhimu kama vile Mtazamo Usioegemea Upande Wowote na Uthibitishwaji.

Kozi hii ni ya maelezo na vitendo, ambapo wanafunzi watapewa mazoezi halisi ya kuhariri makala mbalimbali. Pia, wataelekezwa jinsi ya kuchangia kwenye miradi ya Wikimedia kwa njia endelevu na yenye athari chanya.

Malengo ya Kozi:

  • Kuwezesha wanafunzi kuwa wachangiaji waaminifu na wa kitaalamu wa Wikipedia.
  • Kujenga uelewa wa umuhimu wa maarifa ya wazi kwa maendeleo ya jamii.

Kundi lengwa:
Kozi hii inafaa kwa wanafunzi wa sekondari, vyuo vikuu, na mtu yeyote anayetaka kuchangia maarifa kwenye Wikipedia.

Muda:
Kozi hii itafanyika kwa muda wa wiki 8, mara 3 kwa wiki.

Makala hii imetoholewa kutoka EduWiki Dashboard.

Show More

Course Content

Sera za Wikipedia
Sera za Wikipedia zinaweka msingi wa jinsi watumiaji wanavyoshirikiana na jinsi maudhui yanavyoundwa. Katika sehemu hii, utajifunza kuhusu sera muhimu kama Mtazamo Usioegemea Upande Wowote, Uthibitishwaji, na Hakimiliki ya Maudhui, ambazo husaidia kudumisha ubora na uaminifu wa makala.

  • Nguzo Tano za Wikipedia.
  • Nguzo ya kwanza
  • Nguzo ya pili
  • Nguzo ya tatu.
  • Nguzo ya Nne.
  • Nguzo ya Tano.
  • Mapitio.
  • Kipimo cha Nguzo Tano
  • Hongera!
  • Uthibitishaji.
  • Kipimo cha Uthibitishaji
  • Umaarufu
  • Umaarufu (mwendelezo…)
  • Kipimo cha Umaarufu
  • Hauhitaji utafiti wa awali.
  • Mfano wa hakuna utafiti wa awali unaohitajika.
  • Haki Miliki na wizi wa maandishi (plagiarism)
  • Mapitio.
  • Tujikumbushe!
  • Jarabio: Sera za Wikipedia
  • Jarabio: Sera za Wikipedia
  • Kazi ya vitendo

Kurasa za Majadiliano
Nyuma ya kila makala nzuri ya Wikipedia kuna wanawikipedia wanaofanya kazi pamoja kuiboresha. Wanawikipedia hawa hujadili juu ya ubora wa kazi hizi kupitia “Ukurasa wa Majadiliano.” Kila makala ya Wikipedia ina Ukurasa wake wa Majadiliano. Hapa ndipo mazungumzo kuhusu makala hufanyika. Kabla ya kuanza kuhariri makala iliyopo, angalia Ukurasa wa Majadiliano. Utapata mwanga juu ya mijadala inayoendelea. Ukurasa wa Majadiliano ni sehemu nzuri ya kutambulisha mipango yako ya kuboresha makala hiyo. Unapopanga kuanza kuandika, shiriki vitabu au makala unazotaka kutumia kuboresha makala hiyo, na uliza maswali ikiwa unayo. Wanawikipedia wenye shauku na mada hiyo mara nyingi watachukua hatua na kujaribu kusaidia. Ni vizuri kuchapisha mawazo yako kabla ya kufanya mabadiliko, lakini si lazima usubiri “ruhusa” kufanya mabadiliko. Kumbuka: Kuwa na ujasiri! Wanawikipedia hutarajia kuwa utasoma ujumbe unaoachwa katika Ukurasa wako wa Majadiliano wa mtumiaji na Ukurasa wa Majadiliano wa makala. Unaweza pia kutumia kurasa hizi kuacha ujumbe kwa wengine. Katika mafunzo yanayofuata, utajifunza jinsi ya kuacha ujumbe kwenye Ukurasa wa Majadiliano.

Kuwasiliana na Wengine Kwenye Wikipedia
Ushirikiano ni muhimu katika jukwaa hili la wazi. Katika sehemu hii, utajifunza jinsi ya kushiriki mawazo, kuuliza maswali, na kutoa maoni kwa njia ya heshima kupitia zana kama kurasa za majadiliano na vikundi vya jamii.

Kutathmini Makala na Vyanzo
Ubora wa makala za Wikipedia unategemea uhalali wa vyanzo vilivyotumika. Utajifunza mbinu za kutathmini makala na vyanzo ili kuhakikisha kuwa taarifa ni za kweli na za kuaminika.

Kupata Makala Yako
Hatua ya kwanza ya kuchangia kwenye Wikipedia ni kuchagua mada inayokufaa. Sehemu hii itakusaidia kutafuta makala ambazo zinaweza kuhitaji maboresho au kuanza mpya kulingana na maslahi yako.

Kuboresha Uwakilishi Kwenye Wikipedia
Wikipedia inalenga kuwa jukwaa la usawa wa maarifa. Utajifunza mbinu za kuboresha uwakilishi wa makundi, tamaduni, na masuala ambayo yanaweza kuwa yameachwa au kupuuzwa.

Kufanya Kazi Moja kwa Moja Kwenye Wikipedia.
Sehemu hii inakusaidia kuelewa jinsi ya kufanya mabadiliko ya moja kwa moja kwenye makala za Wikipedia, kwa kuzingatia taratibu za uhariri na miongozo ya jamii.

Kuchangia Picha na Faili.
Wikipedia ni zaidi ya maneno. Utajifunza jinsi ya kuongeza picha, video, na faili zingine za Commons ili kuboresha maudhui ya makala.

Kutafsiri Makala
Wikipedia ni jukwaa la kimataifa. Katika sehemu hii, utajifunza jinsi ya kutafsiri makala kutoka lugha moja kwenda nyingine, huku ukizingatia miongozo ya tafsiri.

Kuongeza Marejeo
Marejeo yanahakikisha uhalali wa maudhui. Utajifunza jinsi ya kuongeza marejeleo kwa kutumia vyanzo vya kuaminika ili kuthibitisha taarifa unazochangia.

Wizi wa Maandishi na Uvunjaji wa Hakimiliki
Sehemu hii inalenga kukuongoza jinsi ya kuepuka wizi wa maandishi na uvunjaji wa hakimiliki kwa kuhakikisha kazi yako ni ya kipekee na kufuata sheria za maudhui ya wazi.

Student Ratings & Reviews

No Review Yet
No Review Yet

Want to receive push notifications for all major on-site activities?